Mapema hivi leo tumeadhimisha siku ya Afya na Usafi wa Hedhi mwaka huu katika Shule ya Msingi Kizurini katika Kaunti Ndogo ya Kaloleni.
Hafla hiyo, iliyofanyika chini ya maudhui “Pamoja kwa Kilifi inayokumbatia afya Na usafi wa hedhi”ilijumuisha usambazaji wa sodo za usafi na mashindano ya kandanda ya jinsia tofauti.
Serikali ya Kaunti ya Kilifi kwa sasa iko mbioni kuandaa sera ya Afya na Usafi wa hedhi kwa lengo la kutoa sodo za usafi na elimu kuhusu usafi wa hedhi kwa wasichana wanaobalehe. Lengo letu ni kuwezesha majadiliano ya wazi katika maeneo salama na kutoa msaada, ikiwa ni pamoja na bidhaa za hedhi, kwa wasichana wadogo.
Tunawasihi wakazi wote wa Kilifi kushiriki katika mazungumzo kuhusu suala hili na kuwawezesha wanawake na wasichana wetu kupata hedhi kwa heshima, bila aibu au hofu. Ukosefu wa ufahamu umesababisha wasichana wadogo kushiriki katika shughuli hatari zinazozuia matarajio yao ya baadaye.