Nilijumuika na Naibu Gavana, Mheshimiwa Flora Mbetsa Chibule, Mama wa kwanza wa Kilifi, Mheshimiwa Sussane Mung’aro, Mawaziri wenzangu pamoja na wananchi wa Kilifi katika eneo la Mwarakaya kusherekea siku ya kimataifa ya wanawake ulimwenguni.
Nilitumia fursa hii kutambua mafanikio ya wanawake kupitia kwa uongozi wa Gavana Gideon Mung’aro, ambapo baadhi ya akina mama wachanga pamoja na wajane wamekuwa wakifaidika kwa kulipiwa karo kusoma katika vyuo vya kiufundi pamoja na hata kupitia michezo ambapo wasichana wetu sasa watapata fursa ya kuajiriwa kupitia kwa mashindano ya Governor’s Cup.
Aidha, tunazidi kuwaunganisha wanawake wa Kilifi na rasilimali za kifedha kupitia kwa hazina ya Wezesha Fund ili kuwasaidia kukidhi mahitaji yao ya msingi na kuanzisha au kukuza biashara.
Naamini kwa pamoja, tutazidi kumuinua mwanamke wa Kilifi hata zaidi.